6 Enyi wazawa wa Esau, mali zenu zimetekwa;hazina zenu zote zimeporwa!
7 Washirika wenzenu wamewadanganya,wamewafukuza nchini mwenu.Mliopatana nao wamewashinda vitani,rafiki wa kutegemewa ndio waliokutegea mitego,nawe hukuelewa yaliyokuwa yanatendeka.
8 Mimi Mwenyezi-Mungu nakuuliza hivi:Je, siku hiyo, sitawaangamiza wenye hekima kutoka Edomuna wenye maarifa kutoka mlima Esau?
9 Ewe Temani, mashujaa wako watatishikana kila mtu atauawa mlimani Esau.
10 “Kwa sababu ya matendo maovumliyowatendea ndugu zenu wazawa wa Yakobo,mtaaibishwa na kuangamizwa milele.
11 Siku ile mlisimama kando mkitazama tu,wakati wageni walipopora utajiri wao,naam, wageni walipoingia malango yaona kugawana utajiri wa Yerusalemu kwa kura.Kwa hiyo nanyi mlitenda kama wazawa wao.
12 Msingalifurahia siku hiyo ndugu zenu walipokumbwa na mikasa;msingaliwacheka Wayudana kuona fahari wakati walipoangamizwa;msingalijigamba wenzenu walipokuwa wanataabika.