1 Hakika u mzuri ewe mpenzi wangu,hakika u mzuri!Macho yako ni kama ya huanyuma ya shela lako,nywele zako ni kama kundi la mbuziwashukao katika milima ya Gileadi.
2 Meno yako ni kama kondoo majike waliokatwa manyoyawanaoteremka baada ya kuogeshwa.Kila mmoja amezaa mapacha,na hakuna yeyote aliyefiwa.
3 Midomo yako ni kama utepe mwekundu,kinywa chako chavutia kweli.Nyuma ya shela lako,mashavu yako ni kama nusu mbili za komamanga.
4 Shingo yako ni kama mnara wa Daudi,uliojengwa ili kuhifadhia silaha,ambako zimetundikwa ngao elfu mojazote zikiwa za mashujaa.
5 Matiti yako ni kama paa mapacha,ambao huchungwa penye yungiyungi.
6 Nitakaa kwenye mlima wa manemane,na kwenye kilima cha ubani,hadi hapo kutakapopambazuka,na giza kutoweka.