18 Yahasa, Kedemothi, Mefaathi,
19 Kiriathaimu, Sibma, Sereth-shahari, huko kilimani bondeni,
20 Beth-peori, miteremko ya mlima Pisga, Beth-yeshimothi
21 na miji yote ya tambarare, nchi yote ya mfalme Sihoni wa Waamori ambaye alitawala huko Heshboni; Mose alikuwa amemshinda huyu Sihoni pamoja na viongozi wa Midiani, Evi, Rekemu, Suri, Huri na Reba, ambao walitawala nchi kwa niaba ya mfalme Sihoni.
22 Balaamu, mtabiri, mwana wa Beori ambaye Waisraeli walimuua alikuwa mmoja wao.
23 Mpaka wa nchi ya kabila la Reubeni upande wa magharibi ulikuwa mto Yordani. Miji na maeneo yaliyotajwa hapa ndiyo sehemu waliyopewa watu wa koo za kabila la Reubeni.
24 Sehemu ya nchi ambayo Mose aliwapa watu wa kabila la Gadi kulingana na koo zao