28 Miji na vijiji hivyo ndivyo walivyopewa watu wa kabila la Gadi kulingana na koo zao.
29 Tena, Mose alikuwa ameipatia nusu ya kabila la Manase kulingana na koo zake,
30 eneo la nchi kuanzia Mahanaimu hadi kuingia katika nchi yote iliyokuwa ya mfalme Ogu katika Bashani, pamoja na miji sitini ya Yairi,
31 nusu ya Gileadi, Ashtarothi, Edrei, ambayo ilikuwa chini ya himaya ya mfalme Ogu wa Bashani; Eneo hili walipewa nusu ya wazawa wa Makiri mwana wa Manase, kulingana na koo zao.
32 Mose alikuwa amewagawia sehemu hizo mbalimbali za nchi iliyokuwa mashariki ya Yeriko na Yordani, wakati alipokuwa kwenye tambarare za Moabu.
33 Lakini kabila la Lawi, Mose hakulipa sehemu yao ya nchi, maana aliwaambia kwamba sehemu yao itakuwa kumhudumia Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli.