11 na watu wote walipokwisha vuka, wale makuhani wakawatangulia na lile sanduku la agano la Mwenyezi-Mungu.
12 Wanaume wa kabila la Reubeni na la Gadi na nusu ya kabila la Manase waliwatangulia Waisraeli wakiwa na silaha zao, kama vile walivyoagizwa na Mose.
13 Watu wapatao 40,000 wakiwa na silaha tayari kwa vita walipita mbele ya Mwenyezi-Mungu wakielekea bonde la mji wa Yeriko.
14 Katika siku hiyo Mwenyezi-Mungu akamtukuza Yoshua mbele ya Waisraeli wote, nao wakamheshimu Yoshua maisha yake yote kama walivyomheshimu Mose maishani mwake.
15 Kisha Mwenyezi-Mungu alimwambia Yoshua,
16 “Waamuru makuhani wanaobeba sanduku la maamuzi, watoke mtoni Yordani.”
17 Basi, Yoshua akawaamuru wale makuhani, “Tokeni mtoni Yordani.”