8 Neno la mwisho ni hili; mwe na nia moja, wenye kuhurumiana, wenye kupendana kama ndugu, wasikitikivu, wanyenyekevu;
9 watu wasiolipa baya kwa baya, au laumu kwa laumu; bali wenye kubariki; kwa sababu hayo ndiyo mliyoitiwa ili mrithi baraka.
10 Kwa maana,Atakaye kupenda maisha,Na kuona siku njema,Auzuie ulimi wake usinene mabaya,Na midomo yake isiseme hila.
11 Na aache mabaya, atende mema;Atafute amani, aifuate sana.
12 Kwa kuwa macho ya Bwana huwaelekea wenye haki,Na masikio yake husikiliza maombi yao;Bali uso wa Bwana ni juu ya watenda mabaya.
13 Naye ni nani atakayewadhuru, mkiwa wenye juhudi katika mema?
14 Lakini mjapoteswa kwa sababu ya haki mna heri. Msiogope kutisha kwao, wala msifadhaike; bali mtakaseni Kristo Bwana mioyoni mwenu.