11 Uweza una yeye hata milele na milele. Amina.
12 Kwa mkono wa Silwano, ndugu mwaminifu kama nionavyo, nimewaandikia kwa maneno machache, kuonya na kushuhudia ya kuwa hii ndiyo neema ya kweli ya Mungu. Simameni imara katika hiyo.
13 Mwenzenu mteule hapa Babeli awasalimu, na Marko mwanangu.
14 Salimianeni kwa busu la upendo.Amani na iwe kwenu nyote, mlio katika Kristo. Amina.