12 Lakini huyu, alipokwisha kutoa kwa ajili ya dhambi dhabihu moja idumuyo hata milele, aliketi mkono wa kuume wa Mungu;
13 tangu hapo akingojea hata adui zake wawekwe kuwa chini ya miguu yake.
14 Maana kwa toleo moja amewakamilisha hata milele hao wanaotakaswa.
15 Na Roho Mtakatifu naye amshuhudia; kwa maana, baada ya kusema,
16 Hili ni agano nitakaloagana nao baada ya siku zile, anena Bwana,Nitatia sheria zangu mioyoni mwao,Na katika nia zao nitaziandika;ndipo anenapo,
17 Dhambi zao na uasi wao sitaukumbuka tena kabisa.
18 Basi, ondoleo la hayo likiwapo, hapana toleo tena kwa ajili ya dhambi.