5 Na Musa kweli alikuwa mwaminifu katika nyumba yote ya Mungu kama mtumishi, awe ushuhuda wa mambo yatakayonenwa baadaye;
6 bali Kristo, kama mwana, juu ya nyumba ya Mungu; ambaye nyumba yake ni sisi, kama tukishikamana sana na ujasiri wetu na fahari ya taraja letu mpaka mwisho.
7 Kwa hiyo, kama anenavyo Roho Mtakatifu,Leo, kama mtaisikia sauti yake,
8 Msifanye migumu mioyo yenu,Kama wakati wa kukasirisha,Siku ya kujaribiwa katika jangwa,
9 Hapo baba zenu waliponijaribu, wakanipima,Wakaona matendo yangu miaka arobaini.
10 Kwa hiyo nalichukizwa na kizazi hiki,Nikasema, Sikuzote ni watu waliopotoka mioyo hawa;Hawakuzijua njia zangu;
11 Kama nilivyoapa kwa hasira yangu,Hawataingia rahani mwangu.