1 Basi, ikiwa ikaliko ahadi ya kuingia katika raha yake, na tuogope, mmoja wenu asije akaonekana ameikosa.
2 Maana ni kweli, sisi nasi tumehubiriwa habari njema vile vile kama hao. Lakini neno lile lililosikiwa halikuwafaa hao, kwa sababu halikuchanganyika na imani ndani yao waliosikia.
3 Maana sisi tulioamini tunaingia katika raha ile; kama vile alivyosema,Kama nilivyoapa kwa hasira yangu,Hawataingia rahani mwangu:ijapokuwa zile kazi zilimalizika tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu.
4 Kwa maana ameinena siku ya saba mahali fulani hivi, Mungu alistarehe siku ya saba, akaziacha kazi zake zote;
5 na hapa napo, Hawataingia rahani mwangu.
6 Basi, kwa kuwa neno hili limebaki kwamba wako watu watakaoingia humo, na wale waliohubiriwa habari ile zamani walikosa kuingia kwa sababu ya kuasi kwao,