16 asiyekuwa kuhani kwa sheria ya amri iliyo ya jinsi ya mwili, bali kwa nguvu za uzima usio na ukomo;
17 maana ameshuhudiwa kwamba,Wewe u kuhani mileleKwa mfano wa Melkizedeki.
18 Maana, kuna kubatiliwa kwa ile amri iliyotangulia, kwa sababu ya udhaifu wake, na kutokufaa kwake;
19 (kwa maana ile sheria haikukamilisha neno); na pamoja na hayo kuliingizwa matumaini yaliyo mazuri zaidi, ambayo kwa hayo twamkaribia Mungu.
20 Na kwa kuwa haikuwa pasipo kiapo,
21 (maana wale walifanywa makuhani pasipo kiapo; bali yeye, pamoja na kiapo, kwa yeye aliyemwambia,Bwana ameapa wala hataghairi,Wewe u kuhani milele;)
22 basi kwa kadiri hii Yesu amekuwa mdhamini wa agano lililo bora zaidi.