3 Maana kila kuhani mkuu huwekwa ili atoe vipawa na dhabihu; kwa hiyo lazima huyu naye awe na kitu cha kutoa.
4 Kama angekuwa juu ya nchi, asingekuwa kuhani; maana wako watoao sadaka kama iagizavyo sheria;
5 watumikiao mfano na kivuli cha mambo ya mbinguni, kama Musa alivyoagizwa na Mungu, alipokuwa tayari kuifanya ile hema; maana asema, Angalia ukavifanye vitu vyote kwa mfano ule ulioonyeshwa katika mlima.
6 Lakini sasa amepata huduma iliyo bora zaidi, kwa kadiri alivyo mjumbe wa agano lililo bora, lililoamriwa juu ya ahadi zilizo bora.
7 Maana kama lile la kwanza lingalikuwa halina upungufu, nafasi isingalitafutwa kwa lile la pili.
8 Maana, awalaumupo, asemaAngalia, siku zinakuja, asema Bwana,Nami nitawatimizia nyumba ya Israeli na nyumba ya Yuda agano jipya;
9 Halitakuwa kama agano lile nililoagana na baba zao,Katika siku ile nilipowashika mikono yao niwatoe katika nchi ya Misri.Kwa sababu hawakudumu katika agano langu,Mimi nami sikuwajali asema Bwana.