Flp.
Sura 4:17-23
Swahili Union Version
17Si kwamba nakitamani kile kipawa, bali nayatamani mazao yanayozidi kuwa mengi, katika hesabu yenu.
18Lakini ninavyo vitu vyote na kuzidi, tena nimejaa tele; nimepokea kwa mkono wa Epafrodito vitu vile vilivyotoka kwenu, harufu ya manukato, sadaka yenye kibali, impendezayo Mungu.
19Na Mungu wangu atawajazeni kila mnachokihitaji kwa kadiri ya utajiri wake, katika utukufu, ndani ya Kristo Yesu.
20Sasa atukuzwe Mungu, Baba yetu, milele na milele. Amina.
21Mnisalimie kila mtakatifu katika Kristo Yesu. Ndugu walio pamoja nami wawasalimu.
22Watakatifu wote wawasalimu, hasa wao walio wa nyumbani mwa Kaisari.
23Neema ya Bwana Yesu Kristo na iwe pamoja na roho zenu.