1 Basi watoza ushuru wote na wenye dhambi walikuwa wakimkaribia wamsikilize.
2 Mafarisayo na waandishi wakanung’unika, wakisema, Mtu huyu huwakaribisha wenye dhambi, tena hula nao.
3 Akawaambia mfano huu, akisema,
4 Ni nani kwenu, mwenye kondoo mia, akipotewa na mmojawapo, asiyewaacha wale tisini na kenda nyikani, aende akamtafute yule aliyepotea hata amwone?
5 Naye akiisha kumwona, humweka mabegani pake akifurahi.
6 Na afikapo nyumbani kwake, huwaita rafiki zake na jirani zake, akawaambia, Furahini pamoja nami, kwa kuwa nimekwisha kumpata kondoo wangu aliyepotea.