30 Lakini Mungu akamfufua katika wafu;
31 akaonekana siku nyingi na wale waliopanda naye kutoka Galilaya hata Yerusalemu, ambao sasa ndio walio mashahidi wake mbele ya watu.
32 Na sisi tunawahubiri habari njema ya ahadi ile waliyopewa mababa,
33 ya kwamba Mungu amewatimizia watoto wetu ahadi hiyo, kwa kumfufua Yesu; kama ilivyoandikwa katika Zaburi ya pili,Wewe ndiwe Mwanangu, mimi leo nimekuzaa.
34 Tena ya kuwa alimfufua katika wafu, asipate kurudia uharibifu, amenena hivi,Nitawapa ninyi mambo matakatifu ya Daudi yaliyo amini.
35 Kwa hiyo anena na pengine,Hutamwachia Mtakatifu wako kuona uharibifu.
36 Kwa maana Daudi, akiisha kulitumikia shauri la Mungu katika kizazi chake, alilala, akawekwa pamoja na baba zake, akaona uharibifu.