34 Tena ya kuwa alimfufua katika wafu, asipate kurudia uharibifu, amenena hivi,Nitawapa ninyi mambo matakatifu ya Daudi yaliyo amini.
35 Kwa hiyo anena na pengine,Hutamwachia Mtakatifu wako kuona uharibifu.
36 Kwa maana Daudi, akiisha kulitumikia shauri la Mungu katika kizazi chake, alilala, akawekwa pamoja na baba zake, akaona uharibifu.
37 Bali huyu aliyefufuliwa na Mungu hakuona uharibifu.
38 Basi, na ijulikane kwenu, ndugu zangu, ya kuwa kwa huyo mnahubiriwa msamaha wa dhambi;
39 na kwa yeye kila amwaminiye huhesabiwa haki katika mambo yale yote asiyoweza kuhesabiwa haki kwa torati ya Musa.
40 Angalieni, basi, isiwajilie habari ile iliyonenwa katika manabii.