1 Baada ya siku tano, Anania, Kuhani Mkuu, akatelemka na baadhi ya wazee pamoja naye, na msemi mmoja, Tertulo, nao wakamweleza liwali habari za Paulo.
2 Naye alipoitwa, Tertulo akaanza kumshitaki, akisema,Kwa kuwa mnapata amani nyingi chini yako, Feliki mtukufu, na kwa maangalizi yako mambo mabaya yanatengenezwa kwa ajili ya taifa hili,
3 basi tunayapokea kila wakati na kila mahali, kwa shukrani yote.
4 Lakini nisikuudhi zaidi, nakusihi utusikilize maneno machache kwa fadhili zako.
5 Kwa maana tumemwona mtu huyu mkorofi, mwanzilishi wa fitina katika Wayahudi wote duniani, tena ni kichwa cha madhehebu ya Wanazorayo.
6 Na tena alijaribu kulitia hekalu unajisi; tukamkamata; [tukataka kumhukumu kwa sheria yetu.