15 tena wawe na amri ya kutoa pepo.
16 Akawaweka wale Thenashara; na Simoni akampa jina la Petro;
17 na Yakobo, mwana wa Zebedayo, na Yohana nduguye Yakobo, akawapa jina la Boanerge, maana yake, wana wa ngurumo;
18 na Andrea, na Filipo, na Bartholomayo, na Mathayo, na Tomaso, na Yakobo wa Alfayo, na Thadayo, na Simoni Mkananayo,
19 na Yuda Iskariote, ndiye aliyemsaliti.Kisha akaingia nyumbani.
20 Mkutano wakakusanyika tena, hata wao wenyewe wasiweze hata kula mkate.
21 Jamaa zake walipopata habari wakatoka kwenda kumkamata; maana walisema, Amerukwa na akili.