25 Kwa maana mwenye kitu atapewa, naye asiye na kitu, hata kile alicho nacho atanyang’anywa.
26 Akasema, Ufalme wa Mungu, mfano wake ni kama mtu aliyemwaga mbegu juu ya nchi;
27 akawa akilala na kuondoka, usiku na mchana, nayo mbegu ikamea na kukua, asivyojua yeye.
28 Maana nchi huzaa yenyewe; kwanza jani, tena suke, kisha ngano pevu katika suke.
29 Hata matunda yakiiva, mara atapeleka mundu, kwa kuwa mavuno yamefika.
30 Akasema, Tuulinganishe na nini ufalme wa Mungu? Au tuutie katika mfano gani?
31 Ni kama punje ya haradali, ambayo ipandwapo katika nchi, ingawa ni ndogo kuliko mbegu zote zilizo katika nchi,