53 Hata walipokwisha kuvuka, walifika nchi ya Genesareti, wakatia nanga.
54 Nao wakiisha kutoka mashuani, mara watu walimtambua,
55 wakaenda mbio, wakizunguka nchi ile yote, wakaanza kuwachukua vitandani walio hawawezi, kwenda kila mahali waliposikia kwamba yupo.
56 Na kila alikokwenda, akiingia vijijini, au mijini, au mashambani, wakawaweka wagonjwa sokoni, wakamsihi waguse ngaa pindo la vazi lake; nao wote waliomgusa wakapon