2 Nikaona malaika mwingine, akipanda kutoka maawio ya jua, mwenye muhuri ya Mungu aliye hai; akawapigia kelele kwa sauti kuu wale malaika wanne waliopewa kuidhuru nchi na bahari,
3 akisema, Msiidhuru nchi, wala bahari, wala miti, hata tutakapokwisha kuwatia muhuri watumwa wa Mungu wetu juu ya vipaji vya nyuso zao.
4 Nikasikia hesabu yao waliotiwa muhuri katika kila kabila ya Waisraeli, watu mia na arobaini na nne elfu.
5 Wa kabila ya Yuda kumi na mbili elfu waliotiwa muhuri.Wa kabila ya Reubeni kumi na mbili elfu.Wa kabila ya Gadi kumi na mbili elfu.
6 Wa kabila ya Asheri kumi na mbili elfu.Wa kabila ya Naftali kumi na mbili elfu.Wa kabila ya Manase kumi na mbili elfu.
7 Wa kabila ya Simeoni kumi na mbili elfu.Wa kabila ya Lawi kumi na mbili elfu.Wa kabila ya Isakari kumi na mbili elfu.
8 Wa kabila ya Zabuloni kumi na mbili elfu.Wa kabila ya Yusufu kumi na mbili elfu.Wa kabila ya Benyamini kumi na mbili elfu waliotiwa muhuri.