10 Basi wakamwambia, Macho yako yalifumbuliwaje?
11 Yeye akajibu, Mtu yule aitwaye Yesu alifanya tope, akanipaka macho akaniambia, Nenda Siloamu ukanawe; basi nikaenda na kunawa, nikapata kuona.
12 Wakamwambia, Yuko wapi huyo? Akasema, Mimi sijui.
13 Basi wakampeleka kwa Mafarisayo yule aliyekuwa kipofu zamani.
14 Nayo ilikuwa sabato, hapo Yesu alipofanya zile tope na kumfumbua macho.
15 Basi Mafarisayo nao wakamwuliza tena jinsi gani alivyopata kuona. Akawaambia, Alinitia tope juu ya macho, nami nikanawa, na sasa naona.
16 Basi baadhi ya Mafarisayo wakasema, Mtu huyo hakutoka kwa Mungu, kwa sababu haishiki sabato. Wengine wakasema, Awezaje mtu mwenye dhambi kufanya ishara kama hizo? Kukawa matengano kati yao.