12 Tena Abishai, mwana wa Seruya, akawapiga wa Waedomi katika Bonde la Chumvi watu kumi na nane elfu.
13 Akaweka ngome katika Edomu; na Waedomi wote wakawa watumwa wa Daudi. Naye BWANA akampa Daudi kushinda, kila alikokwenda.
14 Basi Daudi akatawala juu ya Israeli wote; akawafanyia hukumu na haki watu wake wote.
15 Na Yoabu mwana wa Seruya akawa juu ya jeshi; na Yehoshafati mwana wa Ahiludi mwenye kuandika tarehe.
16 Na Sadoki mwana wa Ahitubu, na Ahimeleki mwana wa Abiathari, walikuwa makuhani; na Shausha mwandishi;
17 na Benaya mwana wa Yehoyada alikuwa juu ya Wakerethi na Wapelethi; na wana wa Daudi walikuwa wakuu kumzunguka mfalme.