22 Akafa Eleazari, wala hakuwa na wana, ila binti tu; na ndugu zao, wana wa Kishi, wakawaoa.
23 Wana wa Mushi; Mali, na Ederi, na Yeremothi, watu watatu.
24 Hao walikuwa wana wa Lawi, kwa kufuata mbari za baba zao, yaani, vichwa vya mbari za baba zao waliohesabiwa, kwa hiyo hesabu ya majina yao kwa vichwa, hao walioifanya kazi ya utumishi wa nyumba ya BWANA, wenye miaka ishirini na zaidi.
25 Kwa kuwa Daudi alisema, BWANA, Mungu wa Israeli, amewastarehesha watu wake; naye hukaa Yerusalemu milele;
26 wala Walawi hawahitaji tena kuichukua maskani, na vyombo vyake vyote kwa utumishi wake.
27 Maana kwa maneno ya mwisho ya Daudi, hao wana wa Lawi walihesabiwa, wenye miaka ishirini na zaidi.
28 Kwani kazi yao ilikuwa kuwangojea wana wa Haruni katika utumishi wa nyumba ya BWANA, nyuani, na vyumbani, na kwa kuvisafisha vitakatifu vyote, ndiyo kazi ya utumishi wa nyumba ya Mungu;