21 wa nusu kabila ya Manase katika Gileadi, Ido mwana wa Zekaria; wa Benyamini, Yaasieli mwana wa Abneri;
22 wa Dani, Azareli mwana wa Yerohamu. Hao walikuwa maakida wa kabila za Israeli.
23 Lakini Daudi hakufanya hesabu yao wenye miaka ishirini na waliopungua; kwa kuwa BWANA alikuwa amesema, ya kwamba atawaongeza Israeli mfano wa nyota za mbinguni.
24 Yoabu, mwana wa Seruya, akaanza kuhesabu, lakini hakumaliza; na ghadhabu ikawapata Israeli kwa hayo; wala haikuhesabiwa hesabu hiyo ndani ya taarifa za mfalme Daudi.
25 Na juu ya hazina za mfalme alikuwa Azmawethi mwana wa Adieli; na juu ya hazina za mashambani, za mijini, na vijijini, na ngomeni, alikuwa Yonathani mwana wa Uzia;
26 na juu ya hao wenye kazi ya shamba kuilima ardhi alikuwa Ezri mwana wa Kelubu;
27 na juu ya mashamba ya mizabibu alikuwa Shimei, Mramathi; na juu ya mazao ya mizabibu kwa ghala za mvinyo alikuwa Zabdi, Mshifmi;