77 Nao mabaki ya Walawi, wana wa Merari, wakapewa, katika kabila ya Zabuloni; Rimona pamoja na viunga vyake, na Tabori pamoja na viunga vyake;
78 na ng’ambo ya mto wa Yordani huko Yeriko, upande wa mashariki wa Yordani, katika kabila ya Reubeni; Bezeri katika nyika pamoja na viunga vyake, na Yahasa pamoja na viunga vyake,
79 na Kedemothi pamoja na viunga vyake, na Mefaathi pamoja na viunga vyake;
80 na katika kabila ya Gadi; Ramothi katika Gileadi pamoja na viunga vyake, na Mahanaimu pamoja na viunga vyake;
81 na Heshboni pamoja na viunga vyake, na Yazeri pamoja na viunga vyake.