7 BWANA hufukarisha mtu, naye hutajirisha;Hushusha chini, tena huinua juu.
8 Humwinua mnyonge kutoka mavumbini,Humpandisha mhitaji kutoka jaani,Ili awaketishe pamoja na wakuu,Wakakirithi kiti cha enzi cha utukufu;Kwa maana nguzo za dunia zina BWANA,Naye ameuweka ulimwengu juu yake.
9 Yeye atailinda miguu ya watakatifu wake;Bali waovu watanyamazishwa gizani,Maana kwa nguvu hakuna atakayeshinda;
10 Washindanao na BWANA watapondwa kabisa;Toka mbinguni yeye atawapigia radi;BWANA ataihukumu miisho ya dunia;Naye atampa mfalme wake nguvu,Na kuitukuza pembe ya masihi wake.
11 Kisha Elkana akaenda Rama nyumbani kwake. Na yule mtoto akamtumikia BWANA mbele yake Eli, kuhani.
12 Basi, hao wana wa Eli walikuwa watu wasiofaa kitu; hawakumjali BWANA,
13 wala haki ya makuhani ilivyokuwa kwa watu. Wakati huo mtu ye yote alipotoa dhabihu wakati wo wote, ndipo huja mtumishi wa kuhani, nyama ilipokuwa katika kutokota, naye akawa na uma wa meno matatu mkononi mwake;