15 Ndipo Daudi akamwita mmoja wa vijana, akamwambia, Mwendee, ukamwangukie. Basi akampiga hata akafa.
16 Daudi akamwambia, Damu yako na iwe juu ya kichwa chako mwenyewe; maana umejishuhudia nafsi yako ukisema, Nimemwua masihi wa BWANA.
17 Basi Daudi akamwomboleza Sauli, na Yonathani, mwanawe, maombolezo haya;
18 (kama ilivyoandikwa katika kitabu cha Yashari), akasema,Wana wa Yuda na wafundishwe haya,
19 Walio fahari yako, Ee IsraeliJuu ya mahali pako palipoinuka wameuawa;Jinsi mashujaa walivyoanguka!
20 Msiyahubiri mambo haya katika Gathi,Msiyatangaze katika njia za Ashkeloni;Wasije wakashangilia binti za Wafilisti,Binti za wasiotahiriwa wakasimanga.
21 Enyi milima ya Gilboa, visiwepo juu yenuUmande wala mvua, wala mashamba ya matoleo;Maana ndipo ilipotupwa kwa aibu ngao ya shujaa,Ngao yake Sauli, pasipo kutiwa mafuta.