3 Mungu wa mwamba wangu, nitamwamini yeye;Ngao yangu, na pembe ya wokovu wangu, mnara wangu, namakimbilio yangu;Mwokozi wangu, waniokoa na jeuri.
4 Nitamwita BWANA astahiliye kusifiwa;Hivyo nitaokoka na adui zangu.
5 Maana mawimbi ya mauti yalinizunguka,Mafuriko ya uovu yakanitia hofu.
6 Kamba za kuzimu zilinizunguka;Mitego ya mauti ikanikabili.
7 Katika shida yangu nalimwita BWANA,Naam, nikamlalamikia Mungu wangu;Naye akaisikia sauti yangu hekaluni mwake,Kilio changu kikaingia masikioni mwake.
8 Ndipo nchi ilipotikisika na kutetemeka,Misingi ya mbinguni ikasuka-sukaNa kutikisika, kwa sababu alikuwa na ghadhabu.
9 Kukapanda moshi kutoka puani mwake,Moto ukatoka kinywani mwake ukala;Makaa yakawashwa nao.