7 Katika shida yangu nalimwita BWANA,Naam, nikamlalamikia Mungu wangu;Naye akaisikia sauti yangu hekaluni mwake,Kilio changu kikaingia masikioni mwake.
8 Ndipo nchi ilipotikisika na kutetemeka,Misingi ya mbinguni ikasuka-sukaNa kutikisika, kwa sababu alikuwa na ghadhabu.
9 Kukapanda moshi kutoka puani mwake,Moto ukatoka kinywani mwake ukala;Makaa yakawashwa nao.
10 Aliziinamisha mbingu akashuka;Kukawa na giza kuu chini ya miguu yake.
11 Akapanda juu ya kerubi akaruka;Naam, alionekana juu ya mabawa ya upepo.
12 Akafanya giza hema zake za kumzunguka,Makusanyiko ya maji, mawingu makuu ya mbinguni.
13 Toka mwangaza uliokuwa mbele zakeMakaa ya moto yakawashwa.