1 Basi haya ndiyo maneno ya mwisho ya Daudi.Daudi, mwana wa Yese, anena,Anena huyo mtu aliyeinuliwa juu,Yeye, masihi wake Mungu wa Yakobo,Mtungaji wa nyimbo za Israeli mwenye kupendeza;
2 Roho ya BWANA ilinena ndani yangu,Na neno lake likawa ulimini mwangu.
3 Mungu wa Israeli alisema,Mwamba wa Israeli aliniambia,Atawalaye wanadamu kwa haki,Akitawala katika kicho cha Mungu,
4 Atakuwa kama nuru ya asubuhi jua lichapo,Asubuhi isiyo na mawingu.Lachipuza majani mabichi juu ya nchi,Kwa mwangaza baada ya mvua;
5 Je! Sivyo ilivyo nyumba yangu mbele za BWANA?Kwa kuwa amefanya nami agano la milele;Ina taratibu katika yote, ni thabiti,Maana ni wokovu wangu wote, na shauku langu lote.
6 Lakini hatawachipuza watu wa ubatili;Watakuwa wote kama miiba ya nyikani ya kutupwa,Ambayo haivuniki kwa mkono,