1 Ikawa baada ya mambo hayo, wakati wa kutawala kwake Artashasta, mfalme wa Uajemi, Ezra, mwana wa Seraya, mwana wa Azaria, mwana wa Hilkia,
2 mwana wa Shalumu, mwana wa Sadoki, mwana wa Ahitubu,
3 mwana wa Amaria, mwana wa Azaria, mwana wa Merayothi,
4 mwana wa Zerahia, mwana wa Uzi, mwana wa Buki,
5 mwana wa Abishua, mwana wa Finehasi, mwana wa Eleazari, mwana wa Haruni, kuhani mkuu;
6 huyo Ezra akakwea kutoka Babeli; naye alikuwa mwandishi mwepesi katika sheria ya Musa, aliyokuwa ameitoa BWANA, Mungu wa Israeli; naye mfalme akamjalia matakwa yake yote, kama mkono wa BWANA, Mungu wake, ulivyokuwa pamoja naye.
7 Nao wakakwea baadhi ya wana wa Israeli, na wa makuhani, na wa Walawi, na waimbaji, na mabawabu, na Wanethini, ili kwenda Yerusalemu, katika mwaka wa saba wa mfalme Artashasta.