1 Ndipo Musa na wana wa Israeli wakamwimbia BWANA wimbo huu wakanena, na kusema,Nitamwimbia BWANA, kwa maana ametukuka sana;Farasi na mpanda farasi amewatupa baharini.
2 BWANA ni nguvu zangu, na wimbo wangu;Naye amekuwa wokovu wangu.Yeye ni Mungu wangu, nami nitamsifu;Ni Mungu wa baba yangu, nami nitamtukuza.
3 BWANA ni mtu wa vita,BWANA ndilo jina lake.
4 Magari ya Farao na jeshi lake amewatupa baharini,Maakida yake wateule wamezama katika bahari ya Shamu.
5 Vilindi vimewafunikiza,Walizama vilindini kama jiwe.
6 BWANA, mkono wako wa kuume umepata fahari ya uwezo,BWANA, mkono wako wa kuume wawaseta-seta adui.