23 Maana waliniambia, Katufanyie miungu, itakayokwenda mbele yetu, kwa maana mtu huyo Musa, aliyetutoa katika nchi ya Misri, hatujui yaliyompata.
24 Nikawaambia, Mtu ye yote aliye na dhahabu na aivunje; basi wakanipa, nami nikaitupa ndani ya moto, akatoka ndama huyu.
25 Basi Musa alipoona ya kuwa watu hawa wameasi, maana Haruni amewaacha waasi, ili wawe dhihaka kati ya adui zao,
26 ndipo Musa akasimama katika mlango wa marago, akasema, Mtu awaye yote aliye upande wa BWANA, na aje kwangu. Wana wa Lawi wote wakamkusanyikia
27 Akawaambia, BWANA, Mungu wa Israeli, asema hivi, Kila mtu na ajifunge upanga wake pajani mwake, akapite huko na huko toka mlango hata mlango kati ya marago, mkamchinje kila mtu ndugu yake, na kila mtu mwenziwe na kila mtu jirani yake.
28 Na hao wana wa Lawi wakafanya kama vile alivyosema Musa, wakaanguka siku ile kama watu elfu tatu.
29 Musa akasema, Jiwekeni wakfu kwa BWANA leo, naam, kila mtu juu ya mwanawe na juu ya ndugu yake; ili awape baraka leo.