21 kisha akalileta sanduku akalitia ndani ya maskani, naye akalitundika pazia la sitara, akalisitiri sanduku la ushuhuda; kama BWANA alivyomwamuru Musa.
22 Akaitia meza ndani ya hema ya kukutania, upande wa maskani ulioelekea kaskazini, nje ya pazia.
23 Akaipanga ile mikate juu yake mbele za BWANA; kama BWANA alivyomwamuru Musa.
24 Kisha akakitia kinara cha taa ndani ya hema ya kukutania, kuikabili ile meza, upande wa maskani ulioelekea kusini.
25 Kisha akaziwasha taa zake mbele za BWANA, kama BWANA alivyomwamuru Musa.
26 Akaitia madhabahu ya dhahabu ndani ya hema ya kukutania mbele ya pazia.
27 Akafukiza juu yake uvumba wa manukato kama BWANA alivyomwamuru Musa.