1 Mainzi mafu huvundisha marhamu ya mwuza marashi;Kadhalika upumbavu haba ni mzito kuliko hekima na heshima.
2 Moyo wake mwenye hekima upo upande wa kuume;Bali moyo wake mpumbavu upo mkono wa kushoto.
3 Naam, huyo mpumbavu tena, aendapo njiani, hupungukiwa na fahamu zake; hata humwambia kila mtu ya kuwa yeye ni mpumbavu.
4 Roho yake mtawala ikiinuka kinyume chako,Usiondoke mara mahali pako ulipo;Kwa maana roho ya upole hutuliza machukizo yaliyo makubwa.