13 Mwanzo wa maneno ya kinywa chake ni upuuzi; na mwisho wa usemi wake ni wazimu wenye hatari.
14 Tena, upumbavu huongeza maneno; lakini mwanadamu hajui yatakayokuwako; nayo yatakayokuwa baada yake, ni nani awezaye kumweleza?
15 Kazi yao wapumbavu huwachosha kila mmoja,Maana hajui hata njia ya kuuendea mji.
16 Ole wako, nchi, akiwa mfalme wako ni kijana,Na wakuu wako hula asubuhi!
17 Heri kwako, nchi, mfalme wako akiwa mtoto wa watu,Na wakuu wako hula wakati ufaao, Ili makusudi wapate nguvu, wala si kwa ajili ya ulevi.
18 Kwa sababu ya uvivu paa hunepa;Na kwa utepetevu wa mikono nyumba huvuja.
19 Karamu hufanywa kwa ajili ya kicheko,Na divai huyafurahisha maisha; Na fedha huleta jawabu la mambo yote.