1 Kisha nikarudi na kuona madhalimu yote yanayotendeka chini ya jua; na tazama, machozi yao waliodhulumiwa, ambao walikuwa hawana mfariji; na upande wa wale waliowadhulumu kulikuwa na uwezo, walakini wale walikuwa hawana mfariji.
2 Kwa hiyo nikawasifu wafu waliokwisha kufa kuliko wenye uhai walio hai bado;
3 naam, zaidi ya hao wote nikamwita heri yeye asiyekuwako bado, ambaye hakuyaona mabaya yanayotendeka chini ya jua.
4 Tena nikafikiri amali zote, na kila kazi ya ustadi, ya kwamba inatoka katika mtu kupingana na mwenzake. Hayo nayo ni ubatili na kujilisha upepo.
5 Mpumbavu huikunja mikono yake,Naye hula chakula chake mwenyewe;
6 Heri konzi moja pamoja na utulivu,Kuliko konzi mbili pamoja na taabu;na kujilisha upepo.