2 Heri kuiendea nyumba ya matanga,Kuliko kuiendea nyumba ya karamu. Kwa maana huo ndio mwisho wa wanadamu wote, naye aliye hai atautia moyoni mwake.
3 Huzuni ni afadhali kuliko kicheko,Maana simanzi ya uso ni faida ya moyo.
4 Moyo wake mwenye hekima umo nyumbani mwa matanga, bali moyo wake mpumbavu umo nyumbani mwa furaha.
5 Heri kusikia laumu ya wenye hekima,Kuliko mtu kusikia wimbo wa wapumbavu;
6 Maana kama mlio wa miiba chini ya sufuria,Ndivyo kilivyo kicheko cha mpumbavu.Hayo nayo ni ubatili.
7 Kweli jeuri humpumbaza mwenye hekima,Na rushwa huuharibu ufahamu.
8 Heri mwisho wa neno kuliko mwanzo wake,Na mvumilivu rohoni kuliko mwenye roho ya kiburi.