1 Ni nani aliye kama mwenye hekima;Naye ni nani ajuaye kufasiri neno?Hekima ya mtu humng’ariza uso wake,Na ugumu wa uso wake hubadilika.
2 Mimi nasema hivi, Uishike amri ya mfalme; na hiyo kwa sababu umeapa kwa Mungu.
3 Usifanye haraka kutoka mbele ya uso wake; usiendelee kufanya lililo baya; maana yeye hufanya lo lote limpendezalo.
4 Kwa kuwa neno la mfalme lina nguvu; naye ni nani awezaye kumwambia huyo, Wafanya nini?
5 Aishikaye amri hatajua neno baya;Na moyo wa mwenye hekima hujua wakati na hukumu.
6 Kwa maana kwa kila shauri kuna wakati na hukumu; kwa sababu mashaka ya mwanadamu yaliyo juu yake ni makubwa;
7 kwa kuwa hajui yatakayokuwako; kwa maana ni nani awezaye kumweleza jinsi yatakavyokuwa?