3 Basi hawa ndio wakuu wa jimbo waliokaa Yerusalemu; ila mijini mwa Yuda wakakaa kila mtu katika milki yake mijini mwao, yaani, Israeli, makuhani, na Walawi, na Wanethini, na akina watumwa wa Sulemani.
4 Tena wakakaa Yerusalemu wengine wa wana wa Yuda, na wengine wa wana wa Benyamini.Wa wana wa Yuda; Athaya, mwana wa Uzia, mwana wa Zekaria, mwana wa Amaria, mwana wa Shefatia, mwana wa Mahalaleli, wa wana wa Peresi;
5 na Maaseya, mwana wa Baruki, mwana wa Kolhoze, mwana wa Hazaya, mwana wa Adaya, mwana wa Yoyaribu, mwana wa Zekaria, Mshelani.
6 Wana wa Peresi wote waliokaa Yerusalemu walikuwa watu mia nne sitini na wanane, mashujaa.
7 Na wana wa Benyamini ndio hawa; Salu, mwana wa Meshulamu, mwana wa Yoedi, mwana wa Pedaya, mwana wa Kolaya, mwana wa Maaseva, mwana wa Ithieli, mwana wa Yeshaya.
8 Na baada yake Gabai, Salai, watu mia kenda ishirini na wanane.
9 Na Yoeli, mwana wa Zikri, alikuwa msimamizi wao; na Yuda, mwana wa Hasenua, alikuwa wa pili juu ya mji.