9 Mpenzi wangu, nimekulinganishaNa farasi katika magari ya Farao.
10 Mashavu yako ni mazuri kwa mashada,Shingo yako kwa mikufu ya vito.
11 Tutakufanyizia mashada ya dhahabu,Yenye vifungo vya fedha.
12 Muda mfalme alipoketi juu ya matakia,Nardo yangu ilitoa harufu yake.
13 Mpendwa wangu ni kama mfuko wa manemaneUkilazwa usiku maziwani mwangu.
14 Mpendwa wangu ni kama kishada cha hina,Katika mizabibu huko Engedi.
15 Tazama, u mzuri, mpenzi wangu,U mzuri, macho yako ni kama ya hua.