1 Usiku kitandani nalimtafuta mpendwa wa nafsi yangu,Nalimtafuta, nisimpate.
2 Nikasema, Haya, niondoke nizunguke mjini,Katika njia zake na viwanjani,Nimtafute mpendwa wa nafsi yangu.Nikamtafuta, nisimpate.
3 Walinzi wazungukao mjini waliniona;Je! Mmemwona mpendwa wa nafsi yangu?
4 Kitambo kidogo tu nikiisha kuwaondokea,Nikamwona mpendwa wa nafsi yangu;Nikamshika, nisimwache tena,Hata nilipomleta nyumbani mwa mamangu,Chumbani mwake aliyenizaa.
5 Nawasihi, enyi binti za Yerusalemu,Kwa paa na kwa ayala wa porini,Msiyachochee mapenzi, wala kuyaamsha,Hata yatakapoona vema yenyewe.
6 Ni nani huyu apandaye kutoka nyikani,Mfano wake ni nguzo za moshi;Afukizwa manemane na ubani,Na mavumbi ya manukato yote ya mchuuzi?
7 Tazama, ni machela yake Sulemani;Mashujaa sitini waizunguka,Wa mashujaa wa Israeli.
8 Wote wameshika upanga,Wamehitimu kupigana;Kila mtu anao upanga wake pajaniKwa hofu ya kamsa za usiku.
9 Mfalme Sulemani alijifanyizia machelaYa miti ya Lebanoni;
10 Nguzo zake alizifanyiza za fedha,Na mgongo wake wa dhahabu,Kiti chake kimepambwa urujuani,Gari lake limenakishiwa njumu,Hiba ya binti za Yerusalemu.