11 Maana tazama, kaskazi imepita,Masika imekwisha, imekwenda zake;
12 Maua yatokea katika nchi,Wakati wa kupelea umefika,Na sauti ya mwigo husikiwa kwetu.
13 Mtini wapevusha tini zake,Na mizabibu inachanua,Inatoa harufu yake nzuri;Ondoka, mpenzi wangu, mzuri wangu, uje zako.
14 Hua wangu, mafichoni mwa jabali,Katika sitara za magenge,Nitazame uso wako, nisikie sauti yako,Maana sauti yako ni tamu na uso wako mzuri.
15 Tukamatie mbweha,Wale mbweha wadogo,Waiharibuo mizabibu,Maana mizabibu yetu yachanua.
16 Mpendwa wangu ni wangu, na mimi ni wake;Hulisha kundi lake penye nyinyoro.