3 Kama mpera kati ya miti ya msituni,Kadhalika mpendwa wangu kati ya vijana.Naliketi kivulini mwake kwa furaha,Na matunda yake naliyaonja kuwa matamu.
4 Akanileta mpaka nyumba ya karamu,Na bendera yake juu yangu ni mapenzi.
5 Nishibisheni zabibu, niburudisheni kwa mapera,Kwa maana nimezimia kwa mapenzi.
6 Mkono wake wa kushoto uko chini ya kichwa changu,Nao wa kuume unanikumbatia!
7 Nawasihi, enyi binti za Yerusalemu,Kwa paa na kwa ayala wa porini,Msiyachochee mapenzi, wala kuyaamsha,Hata yatakapoona vema yenyewe.
8 Sikiliza! Ni mpendwa wangu! Tazama, anakuja,Akiruka milimani, akichachawa vilimani.
9 Mpendwa wangu ni kama paa, au ayala.Tazama, asimama nyuma ya ukuta wetu,Achungulia dirishani, atazama kimiani.