5 Nikaondoka nimfungulie mpendwa wangu;Mikono yangu ilidondoza manemane,Na vidole vyangu matone ya manemane,Penye vipini vya komeo.
6 Nalimfungulia mpendwa wangu,Lakini mpendwa wangu amegeuka amepita;(Nimezimia nafsi yangu aliponena),Nikamtafuta, nisimpate,Nikamwita, asiniitikie.
7 Walinzi wazungukao mjini waliniona,Wakanipiga na kunitia jeraha,Walinzi walindao kuta zakeWakaninyang’anya shela yangu.
8 Nawasihi, enyi binti za Yerusalemu,Ninyi mkimwona mpendwa wangu,Ni nini mtakayomwambia?Ya kwamba nazimia kwa mapenzi.
9 Mpendwa wa namna gani ni mpendwa wako,Wewe uliye mzuri katika wanawake,Mpendwa wa namna gani ni mpendwa wako,Hata wewe utusihi hivyo?
10 Mpendwa wangu ni mweupe, tena mwekundu,Mashuhuri miongoni mwa elfu kumi;
11 Kichwa chake ni kama dhahabu safi sana,Nywele zake ni za ukoka, nyeusi kama kunguru;