1 Mpendwa wako amekwenda wapi,Wewe uliye mzuri katika wanawake?Mpendwa wako amegeukia upande upi,Ili tumtafute pamoja nawe?
2 Mpendwa wangu ameshukia bustani yake,Kwenye matuta ya rihani;Ili kulisha penye bustani,Ili kuchuma nyinyoro.
3 Mimi ni wake mpendwa wangu, naye ni wangu,Hulisha kundi lake penye nyinyoro.
4 Mpenzi wangu, u mzuri kama Tirza,Mwenye kupendeza kama Yerusalemu,Wa kutisha kama wenye bendera.
5 Uyageuzie macho yako mbali nami,Kwa maana yamenitisha sana.Nywele zako ni kama kundi la mbuzi,Wakijilaza mbavuni pa Gileadi.
6 Meno yako kama kundi la kondoo,Wakipanda kutoka kuoshwa;Ambao kila mmoja amezaa mapacha,Wala hakuna aliyefiwa kati yao.
7 Mashavu yako ni kama kipande cha komamanga,Nyuma ya barakoa yako.