3 Mimi ni wake mpendwa wangu, naye ni wangu,Hulisha kundi lake penye nyinyoro.
4 Mpenzi wangu, u mzuri kama Tirza,Mwenye kupendeza kama Yerusalemu,Wa kutisha kama wenye bendera.
5 Uyageuzie macho yako mbali nami,Kwa maana yamenitisha sana.Nywele zako ni kama kundi la mbuzi,Wakijilaza mbavuni pa Gileadi.
6 Meno yako kama kundi la kondoo,Wakipanda kutoka kuoshwa;Ambao kila mmoja amezaa mapacha,Wala hakuna aliyefiwa kati yao.
7 Mashavu yako ni kama kipande cha komamanga,Nyuma ya barakoa yako.
8 Wako malkia sitini, na masuria themanini,Na wanawali wasiohesabika;
9 Hua wangu, mkamilifu wangu, ni mmoja tu,Mtoto wa pekee wa mamaye.Ndiye kipenzi chake aliyemzaa,Binti wakamwona wakamwita heri;Malkia na masuria nao wakamwona,Wakamsifu, wakisema,