1 Siti msharifu, jinsi zilivyo nzuriHatua zako katika mitalawanda.Mapaja yako ya mviringo ni kama johari,Kazi ya mikono ya fundi mstadi;
2 Kitovu chako ni kama bilauri iliyoviringana,Na isikose divai iliyochanganyika;Tumbo lako ni mfano wa chungu ya ngano,Iliyozungukwa na ugo wa nyinyoro;
3 Maziwa yako mawili ni kama wana-paa wawili,Ambao ni mapacha ya paa;
4 Shingo yako ni kama huo mnara wa pembe;Macho yako kama viziwa vya Heshboni,Karibu na mlango wa Beth-rabi;Pua yako ni kama mnara wa Lebanoni,Unaoelekea Dameski;