2 Kitovu chako ni kama bilauri iliyoviringana,Na isikose divai iliyochanganyika;Tumbo lako ni mfano wa chungu ya ngano,Iliyozungukwa na ugo wa nyinyoro;
3 Maziwa yako mawili ni kama wana-paa wawili,Ambao ni mapacha ya paa;
4 Shingo yako ni kama huo mnara wa pembe;Macho yako kama viziwa vya Heshboni,Karibu na mlango wa Beth-rabi;Pua yako ni kama mnara wa Lebanoni,Unaoelekea Dameski;
5 Kichwa chako juu yako ni kama Karmeli,Na nywele za kichwa chako kama urujuani,Mfalme amenaswa na mashungu yake.
6 Jinsi yalivyo mazuri, yalivyo matamu,Mapenzi katikati ya anasa!
7 Kimo chako kimefanana na mtende,Na maziwa yako na vichala.
8 Nilisema, Nitapanda huo mtende,Na kuyashika makuti yake.Maziwa yako na yawe kama vichala vya mzabibu,Na harufu ya pumzi yako kama mapera;